On 20.7.17

Katibu wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi za Mamlaka hiyo kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 24-26 Julai, 2017 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu.

Wasaili wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 24 Julai, 2017 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo, muda wa usaili umeainishwa kwa kila Kada.

ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.

iii. W a s a i l i w a w a n a t a k i w a k ufika na Vyeti Halisi vya kuanzia  kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

iv. Wasailiwa watakaokosa Vyeti halisi na badala yake kuwasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM
VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

v. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

vi. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanya usaili.

vii. Kila Msailiwa afike na picha yake ‘passport size’

viii. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA)

ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.

ORODHA YA MAJINA 

Receive New Jobs everyday to your inbox. New Jobs Tanzania.

Next
« Prev Post
Previous
Next Post »