On 25.7.17

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri katika Wizara mbalimbali Serikalini anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi (150) za DEREVA DARAJA LA II.

1.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER) – NAFASI 150

1.1MAJUKUMU YA KAZI
I. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
II. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
III. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari,
IV. Kukusafanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
V. Kujanza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
VI. Kufanya usafi wa gari,
VII. Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

1.2SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

1.3MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Agosti, 2017.
xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayatafanyiwa kazi.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://ift.tt/1CAr2Oq
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU (ATTACH YOUR APPLICATION LETTER AND OTHER ACADEMIC CERTIFICATES).

ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.
Receive New Jobs everyday to your inbox. New Jobs Tanzania.

Next
« Prev Post
Previous
Next Post »