On 24.7.17

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA KWA WASAIDIZI WA HESABU KATIKA VITUO VYA AFYA KATIKA MANISPAA YA UBUNGO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa Kama ifuatavyo:-

Msaidizi wa Hesabu Daraja la II X 3

SIFA:
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulikajja Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

KAZI NAMAJUKUMU:
i)Kuandika na kutunza "register" zinazohusu shughuli za uhasibu.
ii) Kutunza kurnbukurnbu zahesabu.
iii) Kupeleka barua/nyaraka za Uhasibu benki.
iv) Kufanya Kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu

NGAZI YA MSHAHARA - TGS.B -Shilingi 390,000/-

MASHARTI YA JUMLA:
• Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania,
• Awe amehitimu na Kupata Cheti cha Taaluma cha kidato cha Nne (IV) NB. Results Slip hazikubaliki
• Awe na Cheti cha Kuzaliwa
• Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo;-
i) Nakala za Vyeti Vya Mwombaji Vilivyothibitishwa,
ii) Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae),
iii) Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.

Kila Mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka18- 45
Waombaji wenye Sifa Pungufu au zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.

Barua ambazo hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu (i-iii) hazitashughulikiwa.

Barua zote za maombi ziandikwe Kwa mkono, zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatavyo:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA YA UBUNGO
S.L.P 55068,
DAR ES SALAAM
TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI:
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05.08.2017 saa 9.30 Alasiri
Ally J. Ally
KAIMU MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA YA UBUNGO

Receive New Jobs everyday to your inbox. New Jobs Tanzania.

Next
« Prev Post
Previous
Next Post »